URASIMU WACHANGIA VIWANDA BUBU VYA MAFUTA MKOANI KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

IMEFAHAMIKA kuwa, Changamoto ya urasimu katika upatikanaji wa leseni ya kuanzisha biashara  ya mafuta na vilainishi vya vyombo vya moto, imechangia  utumiaji wa  mafuta kwa njia ya madumu ambayo  uchakachuliwa na kuuzwa kwa bei nafuu ,huku serikali ikikosa mapato stahiki katika biashara hiyo.

Pia ,baada ya kugundua kuna uingizwaji na utengenezwaji wa virainishi visivyo na ubora  Mamlaka husika (Ewura ) wametoa mafunzo kwa wafanyabiashara nchini hali iliyopunguza uchakachuaji  kutoka 80% hadi kufikia 5% mpaka leo,ilihali wanaendelea kuelimisha walengwa  hususani waishio mikoa ya pembezoni na  hasa vijijini ambao wengi wao ndio watumiaji wa  mafuta hayo.

Akifafanua hilo Meneja wa kampuni ya mafuta ya Hi-Energy ya wilayani Kasulu Feisal Muktar alieleza kuwa, kero ya urasimu dhidi ya leseni ya biashara ya  mafuta ya kuendesha mitambo na vyombo vya moto ni kikwazo kwao,hali inayofanyika kwa ujanja ujanja kwa baadhi ya wafanyabiashara kuendesha biashara hiyo bila kibali husika.

“kitendo hicho kinachangia wanaofanya biashara hii kwa vibali mtambukwa,kunyonywa na wasio na leseni na wanaochakachua vilainishi na mafuta kwa njia ya madumu kupata faida kubwa kwa kuwa hawalipi ushuru na watumiaji wananunua kwa kuwa ni  bei ya kutupa, EWURA wajibikeni kwenye hili” alilalamika Muktar.

Akijibia kero hiyo jana kigoma Ujiji , kwenye mafunzo  ya kuzuia matumizi ya virainishi visivyo na viwango vya ubora na kuelekeza namna ya uzwaji wa bidhaa hiyo,Mkurugenzi wa Petrolia  kutoka Ewura Godwin Samueli akiri athari ipo kwa wafanyabiashara wa vijijini  kuanzisha viwanda bubu.
“tabia ya kuanzisha viwanda vya uchakataji wa vilainishi bila kufuata taratibu hali inayochangia kutumia zana duni na kwa kuwa haijasajiliwa  serikali inakosa mapato huku vyombo vya moto vinaharibiwa miundombinu yake kwa kuwa hakuna ubora katika vilainishi hivyo” alifafanua Meneja huyo.

Aliwakumbusha wanufaika wa mafunzo hayo kuwa,baada ya mafunzo hayo,hwana budi kwedna kwa wakala wa Ewura mkoani kigoma ili,kupata kibali cha kuendesha biashara hiyo ya mafuta sanjari na uchanganyaji wa vilainishi vya kuendeshea mitambo na vyombo vya moto na atakayebainika kwenda kinyume cha sheria,kanuni na taratibu mtambukwa atawajibishwa  kisheria.

0 comments: