UN YAKOSOA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU KATIKA NCHI ZA KIARABU

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika katika nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres ambaye amehutubia kikao cha 34 baraza hilo mjini Geneva amekosoa vikali ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na kutahadharisha kuhusu upuuzwaji wa haki za binadamu. Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi linaundwa na nchi za Saudi Arabia, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Oman na Bahrain. 
Wapinzani na wanaharakati wanauawa au kufungwa hela Bahrain
Vilevile mwakilishi wa Uholanzi katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa amezikosoa nchi zinazopuuza mchango na nafasi ya watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Kiarabu hususan Bahrain na kutoa wito wa kuwepo ushirikiano katika uwanja huo.
Wakati huo huo taasisi na jumuiya za kutetea haki za binadamu likiwemo shirika la Human Rights Watch zimezitaka nchi wanachama na watazamaji katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kutoa taarifa ya pamoja kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika nchini Bahrain. Vilevile yametoa wito wa kuboreshwa haki za binadamu nchini humo.

0 comments: