HATIMAYE mkutano mkuu wa Chama cha
Mawakili Tanganyika, (TLS), umemchagua mwanasheria machachari nchini,
Tundu Lissu, kuwa Rais wa chama hicho.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa. (AICC), jijini Arusha Machi 18,
2017, Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa CHADEMA, amejinyakulia
jumla ya kura 1,411 sawa na asilimia 88% ya kura zote 1,682,
zilizopigwa.
Mbali na Lissu wagombea wengine waliokuwa wakichuana na Lissu ni Victoria Mandari,Francis Stolla na Godwin Mwapongo.
Aidha wakili Godwin Ngwilimi ambaye
aliwahi kuwa Mwanasheria wa TANESCO amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais na
Magai kuwa Mweka hazina.
Aidha imewachagua mawakili saba kuwa wajumbe wa Baraza la TLS ambao ni
Jeremiah Motebesya,Gida Lambaji
,Hussein Mtembwa
,Aisha Sinda, Steven Axweso,David Shilatu
na Daniel Bushele.
Uchaguzi wa TLS mwaka huu umetupa
mafunzo mengi kwa wale tunaopenda kujifunza kuwa wànasheria ni watu
wenye misimamo yao na siyo kazi rahisi kuwayumbisha kwasababu
wanafahamu sheria na haki zao.
Pia TLS imejikuta ikipata umaarufu na
kujulikana kwa watu waliokuwa hawaifahamu TLS kutokana Rais John
Magufuli katika moja ya hotuba yake kuinyoshea kidole TLS wakati tayari
Kamati ya uchaguzi ilikuwa imeishapitisha majina ya wagombea ambao
wamegiwa kura leo,Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrisso Mwakyembe kutoa
tamko lq kutishia kuifuta TLS kwasababu inai ngiza siasa,baadhi ya
wafuasi wa CCM nao waliibuka mitandaoni wakimtuhumu Lissu azuiwe
kugombea TLS maana ataleta siasa TLS .
Na wale wafuasi wa Chadema na makundi
mengine yaliyokuwa yakimuunga mkono Lissu yalimkingia kifua Lissu
wakisema anafaa na kwamba hata baadhi ya wagombea TLS ni wanachama CCM.
Aidha kitendo cha mawakili
wawili,Onesmo Mpenzile na Godfrey Wasonga kufungua kesi za kuzuia
uchaguzi wa TLS usifanyike leo zilizokuwa zimefunguliwa katika Mahakama
Kuu Dodoma,Dar es Salaam ambazo zote hizo mbili mahakama ilizitupila
mbali nazo zilisaidia kuitangaza TLS bila gharama za kulipia matangazo.
Lissu akiwa na mkewe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: