TEMESA YAKABIDHIWA BOTI NNE ZA KISASA BAADA YA UJENZI WAKE KUKAMILIKA

 Boti Mpya ya MV Bweni iliyokabidhiwa kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria nane na itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Kilambo Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Mwanza
(TEMESA Mwanza)

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ukodishaji na Huduma za Vivuko TEMESA Mhandisi Japhet Maselle, nyuma yao ni Meneja wa TEMESA mkoani Mwanza Mhandisi Ferdnand Mishamo wakati wa majaribio ya boti Mpya ya MV Mkongo  iliyojengwa kwa ajili ya kutumika katika eneo la Utete
Rufiji Mkoani Pwani. Boti hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 40.
 Boti tatu kati ya nne mpya zilizokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika wa ujenzi wake. Makabidhiano yamefanyikia jijini Mwanza na boti hizo zitasafirishwa kuelekea Pangani Tanga, Kilambo Mtwara na Msangamkuu Mtwara ili zianze kutoa huduma kwa wananchi.

    Boti Mpya ya MV Kuchele iliyokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na
Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.
Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria nane na
itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Msangamkuu Mtwara.
Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Mwanza.
 Boti Mpya ya MV Tangazo  iliyokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na
Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria 25 na itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Kilambo Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Mwanza.Na

Theresia Mwami – TEMESA Mwanza

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu, jana amepokea boti nne zilizokuwa zikijengwa na kampuni ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza. Dkt. Mgwatu amesema kukamilika kwa boti hizi ni utekelezaji wa ahadi za
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa
alizozitoa kwa wananchi wa Pangani Tanga pamoja na Kilambo na Msangamkuu

Mtwara kwa nyakati tofauti.Dkt. Mgwatu ameongeza kuwa boti hizo nne
zitatoa huduma za dharura hasa wakati wa usiku kwa ajili ya kuhudumia
wagonjwa na pia kutoa usafiri mbadala wakati vivuko vikubwa vinapokuwa
haviwezi kutoa huduma kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupungua
kwa kina cha maji katika maeneo ya Kilambo mkoani Mtwara pamoja na Utete

Mkoani Pwani.Nae Mkurugenzi kutoka kampuni ya Songoro Marine Boatyard
Mhandisi Major Songoro amesema kuwa boti tatu kati ya nne
zilizokabidhidhiwa zimejengwa kwa kutumia “fibre Glass” na boti moja
imejengwa kwa kutumia chuma. Boti ya MV Kuchele ambayo itapelekwa katika
eneo la Msangamkuu Mtwara ina uwezo wa kubeba abiria nane, sawa na boti
ya MV Bweni itakayopelekwa katika eneo la Pangani mkoani Tanga. MV

Mkongo itakayopelekwa Utete mkoani Pwani ina uwezo wa kubeba abiria 40
na MV. Tangazo itakayopelekwa Kilambo/Namoto Mtwara ina uwezo wa kubeba
abiria 25.Aidha Dkt. Mgwatu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa
kuwezesha ujenzi wa boti hizo na tayari amemuagiza mkandarasi huyo
kuhakikisha anazisafirisha boti hizo kwenye maeneo husika haraka
iwezekanavyo ili wanachi waanze kunufaika na huduma mbadala
itakayotolewa na boti hizo. Ujenzi wa boti hizo umefanywa kwa kutumia
fedha za ndani na umegharimu jumla ya shilingi milioni 415.

0 comments: