RC-MWANRI ATAKA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KANDA YA MAGHARIBI WAWE WABUNIFU

 NA MAGNAETH MAGOSSO,KIGOMAN

MWENYEKITI   wa Baraza la uwezeshaji  Uchumi  kwa wananchi Kanda Magharibi ambaye pia ni Mkuu  wa  Mkoa  wa  Tabora Agrey Mwanri amewataka viongozi wa Mikoa na wilaya wawe wabunifu wa fursa  pamoja na kusimamia mifuko ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa wananchi ,ili  kupunguza umaskini kuanzia ngazi ya familia na mkoa kwa ujumla.

Pia amesema  hatapitisha bajeti  ya mwaka wa  fedha  katika halmashauri  ya mkoa wake endapo bajeti haitaonyesha kutengwa kwa  5% ya  fedha za vijana na  5% ya wanawake  kwa ajili ya kuwakopesha kupitia vikundi vyao kwa lengo la kupunguza  kero ya kipato duni.

Aliyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu iliyosimamiwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wa kiuchumi wa wananchi   alieleza kuwa, kitendo cha baadhi ya viongozi  wa  mikoa ,wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuwa miongoni mwa walalamikaji  wa kero mbalimbali  zinazowakabili wananchi ni kutojitambua nafasi zao kwa jamii .

Alifafanua kuwa,kupitia fursa za mikoa yao ni chachu ya kubaini  masoko ya rasilimali zilizopo katika mkoa wake na kupitia tarifa za wadau wa sekta mbalimbali za kiuchumi atajua eneo la kuwawezesha wakulima,wajasiliamali na wafanyabiashara kunufaika na fursa za hapo.        

“viongozi waongoze njia  kwa kubainisha  mahitaji ya masoko mbalimbali  ya kibiashara ,wasimamie mifuko ya uwezeshaji wa wananchi,serikali inajitihada kubwa ya kuwa na uchumi wa viwanda kila kiongozi wa serikali atawambue uwepo wake” alisisitiza Mwanri.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa baraza hilo Beng`I  Issa alisema lengo kubwa ni viongozi kutambua majukumu yao kwa kuwawezesha kiuchumi  wananchi kupitia mifuko ya uwezeshaji katika vikundi vya vijana,wanawake,wajasiliamali na wafanyabiashara kwa ujumla.

Issa alieleza kuwa,washirikishe wadau wa sekta mbalimbali za maendeleo ,ili mifuko ya fedha za umma ziwafikie walengwa  kwa kukopeshwa kupitia vikundi  ili,kuondoa kero ya umaskini kwa wananchi waliowengi na kupitia mafunzo hayo mikoa ya kigoma ,katavi,kagera na Tabora ni wanufaika a mafunzo hayo.

0 comments: