RC KIGOMA ATAKA WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA MIZIGO WAONDOKE KIGOMA

 Na Magreth Magosso,Kigoma
 
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Emanuel  Maganga amewataka wakurugenzi na wakuu wa wilaya wasiowajibika katika kuwaletea wananchi maendeleo wachie nafasi hizo ili wateuliwe wenye uwezo wa kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa Kigoma .
Pia ashangazwa  na baadhi ya viongozi hao kushindwa kuandaa Mpango wa wanufaika wa ujio wa fedha za rais john magufuli ya sh.milioni  hamsini kwa kila kijiji na maeneo ya viwanda ilihali kila wilaya Ina nishati ya umeme.

Maganga alisema hayo jana kigoma Ujiji katika kikao cha kamati ya ushauri Mkoa uliolenga kupitia mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/18 na kusema kuwa, viongozi hao ni wasomi, vijana lakini Elimu yao haiwanufaishi wananchi katika sekta mbalimbali hasa kilimo ambapo wananchi hawapati Huduma ya kilimo cha kisasa.

,,Hakuna kiongozi mgeni, fanyeni kazi ajabu miongoni kwa viongozi mnalima hekari hamsini kwa kutumia trekta lakini hamshirikishi wananchi watumie zana za kisasa katika sekta ya kilimo,, alifafanua mkuu wa Mkoa huo.

Alieleza kuwa, kitendo cha kushindwa kuandaa maeneo ya viwanda na wanufaika wa fedha za rais  ni dalili za ubadhilifu wa fedha na wananchi lengwa kutokunufaika na mamilioni ya rais Magufuli.

Aisha alisema watendaji wengi wa serikali wana Tania ya kuigiza Maisha ya wananchi wenye hitaji la kusaidiwa na serikali yao, lakini changamoto zinazoshindwa kutoweka kutokana na sintofafamu ya watendaji husika kutokuwajibika ipasavyo.

Alisema halmashauri za mkoani hapo zinakabiliwa na kero ya asilimia 5%ya kuwakopesha vijana na 5% ya kuwakopesha wanawake,kimsingi wanawake wa kigoma
Ni wajasiliamali wa uhakika.

Katika kikao hicho kiasi cha fedha sh.bilioni 248.29 zimekadiriwa kutumika katika mwaka 2017/18 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Miradi ya maendeleo ya wananchi.

0 comments: