RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MIEZI MINNE MRADI WA MAJI WA NG’APA MKOANI LINDI UKAMILIKE PIA AKUTANA NA BODI YA WAKURUGENZI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) KATIKA IKULU NDOGO YA LINDI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:50 AM
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa
maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa
Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi
mine na si vinginevyo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika
karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma
Kikwete amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia
wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani
Lindi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wananchi wa Ng’apa mara baada ya kutembelea mradi wa Maji wa eneo hilo
ambao unasuasua kukamilika. Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa
Mkandarasi kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance Private Limited
ya India kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na sio kuleta
visingizio.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu
ndogo Mkoani Lindi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi. Wakwanza
kushoto ni Kiongozi wa Wakurugenzi hao Lekhethe Mmakgoshi kutoka Nchini
Afrika Kusini na Wakwanza kulia ni Mkurugenzi mwingine wa (AfDB)
Dkt.Nyamajeje Weggoro ambaye ni Mtanzania.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Kiongozi wa Wakurugenzi hao kutoka (AfDB) Lekhethe Mmakgoshi mara baada
ya kumaliza mazungumzo na Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Mmoja wa Wakurugenzi wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro mara baada
ya kumaliza mazungumzo na Bodi yao Ikulu ndogo mkoani Lindi.
Sehemu ya
Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa
miezi minne kwa mkandarasi anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika
haraka. (PICHA NA IKULU)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: