Shewiyo, aliendelea kusema akiiomba Selikali kusikia kilio chao kwa kuwaondolea mzigo wa kodi wanao endelea kulipa Serikalini ambapo kituo hicho hakina mfadhili na kinaendeshwa na watu wanaoendelea kujitolea kituoni hapo, Shewiyo, akiwaombea kwa Mungu madaktari hao katika kuwahudumia wananchi kwa ujumla.
PADRI WA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU AIOMBA SERIKALI IWAONDOLEE MZIGO WA KUWALIPIA LESENI MADAKTARI BINGWA WANAOKUJA KUWAFANYIA UPASUAJI WATOTO WA KITANZANIA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:54 PM
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa (kulia) akimfanyia uchunguzi wa Kinywa na meno Shabani Jafari (9) katika Kituo cha Watoto wenye Ulemavu cha Mlali kilichopo Kata ya Mlali, Mkoa wa Dodoma Wilaya ya Kongwa leo, kushoto ni Daktari wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Anold Mtenga.
Na Khamisi Mussa.
PADRI na Mkurugenzi wa Kituo cha watoto Wenye Ulemavu, Paul Shewiyo , amewashukuru Madaktari wa Chama Cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno kwa moyo wao wakujali na kujitolea kwa kuwatembelea watoto wa kituo hicho kwa kutowa Elimu ya upigaji mswaki na utunzani wa kinywa na meno, kuwachunguza na kutibu sambamba na zawadi mbalimbali .
Shewiyo, alisema toka Duni kuumbwa ni kwa mara ya kwanza kituo hicho kutembelewa na madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno, hivyo alipata nafasi ya kuwashukuru na kuendelea kuwawaomba wazidi kutembelea watoto hao na kuomba Jamii kusaidia kituo hicho.
Shewiyo, aliendelea kusema akiiomba Selikali kusikia kilio chao kwa kuwaondolea mzigo wa kodi wanao endelea kulipa Serikalini ambapo kituo hicho hakina mfadhili na kinaendeshwa na watu wanaoendelea kujitolea kituoni hapo, Shewiyo, akiwaombea kwa Mungu madaktari hao katika kuwahudumia wananchi kwa ujumla.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Lorna Carneiro alisema katika
kuelekea Wiki ya Kinywa na Meno ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuongoza
matembezi ya Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno yatakayofanyika mkoani Dodoma Machi 19 mwaka huu, Matembezi
hayo yatafanyika katika Viwanja vya Nyerere Square na kuwashirikisha
wadau mbalimbali wa sekta ya afya na wananchi wa mkoa huo
Sanjari
na matembezi hayo siku itakayofuata Machi 20, ambayo itakuwa ni kilele
cha wiki ya Afya ya Kinywa na Meno Tanzania na Siku ya Afya ya Kinywa na
Meno Duniani, kutakuwa na uchunguzi wa afya ya kinywa ya meno kwa
wananchi bila malipo na katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Lorna Carneiro (aliye chuchumaa) akicheza na mtoto anaye lelewa katika Kituo cha Watoto Wenye ulemavu mara walipofika kutowa huduma kaituoni hapo leo
Watoto wenye ulemavu katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu wakiwa katika chumba chao na mlezi katika kituo hicho
Padri na Mkurugenzi wa Kituo cha watoto Wenye Ulemavu, Paul Shewiyo katika picha ya pamoja na madaktari hao (wa tatu kushoto) wa kwanza kushoto ni Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Lorna Carneiro wa watu kulia ni Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Profesa Bakari Lemmariti onDaktariwa Kinywa na wakwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi na Mhasibu wa Kituo hicho, Paschal Diwi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: