NDEGE MBILI ZA BOMBARDIER ZILIZONUNULIWA NA RAIS DK. MAGUFULI ZAINGIZA SH. BILIONI TISA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:16 PM
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema
wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 katika kipindi cha miezi
minne kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dk. John Pombe
Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai
kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.
Kampuni
ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya
Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air
Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la
Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo
ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na
kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena
Serikalini kwa asilimia 100.
KUTOKA MAKTABA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa na
maafisa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi
ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa
ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe
Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye
ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier
Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam
Jumatano Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: