MKUU WA WILAYA ILALA ATEMBELEA FAMILIA YA MWANAMKE ALIYE ANGUKIWA NA MTI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:12 PM
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameitembelea familia ya mwanamama
aliyeangukiwa na mti katika kibanda chake cha biashara na kupelekea kifo
chake siku mbili zilizopita ambapo chanzo kinatajwa ni mvua ya upepo.
Inatajwa
kuwa mwanamama Zulfa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 48,
alifariki hapohapo baada kuangukiwa na mti huo, ambapo licha ya mvua
hiyo ya upepo kusababisha kifo pia inatajwa kuezua mabati ya baadhi ya
nyumba eneo hilo la kata ya Viwege Bomba Mbili.
DC Mjema ametembelea eneo hilo na kutoa pole kwa familia na kuwaambia kuwa serikali ipo pamoja nao.
Katika
hatua nyingine DC Mjema ametembelea shule ya msingi Kigogo Fresh ambayo
wiki mbili zilizopita ilikubwa na maafa ya mvua kuathiri miundombinu ya
shule hiyo na kupelekea idadi kubwa ya wanafunzi kukosa madarasa ya
kukalia hali iliyopelekea shule kufungwa.
Siku
ya leo DC Mjema ametembelea shule na kushuhudia ukarabati na ujenzi wa
madarasa manne yakiwa yamekamilika jambo ambalo litapelekea zaidi ya
wanafunzi 500 kusoma kwenye madarasa hayo.
Ambapo
pia DC Mjema ameagiza ujenzi wa madarasa mengine mawili ambayo ameahidi
yatakamilika ndani ya miezi miwili na kuleta tumaini jipya kwa
wanafunzi hao, halikadhalika ujenzi wa daraja na barabara jambo litakalo
saidia wanafunzi na wakazi wa eneo hilo kuvuka bila ya kuwa na
wasiwasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: