MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AMESHAURI KUUNDWA KWA KAMATI MAALUM
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:47 AM
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameshauri kuundwa kwa kamati
maalum itakayounda watu watano wenye maono kuhusu suala la mapato,
watatu kutoka kwenye kampuni mbalimbali, na wataalamu kutoka chuo cha
kodi na wengine kutoka chuo cha usimamizi wa fedha IFM, huku wajumbe
wakiwa watumishi wa serikali kwa lengo la kujifunza ili wote kwa pamoja
waje na mikakati ya kukuza mapato katika jiji la Dar es Salaam. RC
Makonda amesema anaamini kamati hiyo italeta suluhisho kwani si
vibaya kujifunza kwa wengine ambao wameendelea kwenye jambo ambalo
linawasumbua wengine, pia amewataka wakuu wa idara kuwajibika na
kufikiria nje ya box kwa kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato na
kuwasumbua viongozi wao wajuu ili pesa zipatikane, akimtolea mfano Rais
Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi alikuwa msumbufu kwa Wizara ya Fedha
ili wampatie fedha za barabara na alifanikiwa hivyo amewataka kuiga
mfano huo. Pia
amesisitiza uwajibikaji kwa watendaji wote kwani kila mtu akifanya
wajibu wake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo maendeleo
yatapatikana. RC
Makonda amezungumzia suala la elimu na kumuagiza Afisa wa elimu wa Mkoa
kuja na mikakati itakayo jibu matokeo mabovu ya elimu kwa Mkoa wa Dar
es Salaam na yaliyojitokeza kipindi hiki yabaki historia kwenye elimu,
na mabadiko yaanze kuonekana kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akifatilia jambo wakati Kikao cha ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilipokuwa kikiendelea Dar es Salaam leo, kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaa Ramadhani Madabida
Baadhi ya viongozi mbalimbali katika Kikao cha ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (katikati) kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa na kushoto ni Katibu Tawala wa Ilala, Edward Mpogolo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: