RC Makonda ameyasema hayo jana, alipokuwa anafungua kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na kuwaomba mameya, madiwani, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuifuatilia miradi hii kwa karibu, huku akishauri kuwa ni vyema miradi hii ikafanyika kwa gharama nafuu, kwa muda mfupi na kwa viwango, kwani fedha za wananchi ndiyo zinatumika wanapaswa kutendewa haki kwa kuona matokeo chanya kwenye miradi ya maendeleo.
Katika hatua nyingine kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited kupitia Mkurugenzi wake Maida Waziri ameeleza kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, haina vumbi wala uterezi na ujenzi wake hutumia muda mfupi na kuishauri serikali kutumia ujenzi huo wa gharama nafuu kwa takribani asilimia 50, huku akizitolea mfano Australia na Algeria kuanza kutumia ujenzi huo, hivyo hiyo ni suluhu ya lawama za muda mrefu kuhusu barabara mbovu nchini.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ujenzi huo wa kibunifu utakuwa njia ya kuvifanya vijiji kuwa miji kupitia barabara.
0 comments: