MAJIBU YA CHINA DHIDI YA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU ILIYOTOLEWA NA MAREKANI

China imejibu ripoti ya Marekani iliyoituhumu nchi hiyo kuwa inakiuka haki za na kuitaja Marekani kuwa ndiyo mkiukaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu duniani.
Ripoti iliyotolewa na China imesema hali ya haki za binadamu nchini Marekani inasikitisha mno.
Ijumaa ya jana Baraza la Serikali ya China lilijibu ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa mwaka jana 2016 na Marekani dhidi yake. Ripoti ya Baraza la Serikali ya Uchina imesema kuwa, Marekani si tu kwamba haizingatii mipaka ya haki za binadamu ndani ya nchi, bali hata nje ya nchi hiyo inakanyaga wazi wazi haki hizo.
Wafungwa waliofurika katika jela za Marekani
Hii si mara ya kwanza ambapo Marekani imekuwa ikiandaa ripoti mbalimbali dhidi ya China ikiituhumu kuwa inakandamiza na kukanyaga haki za binadamu. Watayarishaji wa ripoti ya Baraza la Serikali ya China wanasema kuwa, Marekani inashika nafasi ya pili kwenye orodha ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na wafungwa wengi duniani na kila kati ya watu laki moja wa jamii ya Marekani, 693 wamefungwa jela. Aidha kati ya kila raia wawili wa Marekani, mmoja wao anamiliki silaha ya moto. Ripoti hiyo imeeleza kuwa, zaidi ya kesi elfu 58 za hujuma za silaha za moto zimeripotiwa, ambapo kati ya hizo watu 385 wameuawa kwa silaha hizo.
Sehemu ya wafungwa waliokata tamaa ya maisha huko Marekani
Ukweli ni kwamba, Marekani hakuna haja ya kurejea kwenye takwimu zilizotolewa katika ripoti ya Baraza la Serikali ya China ili kutambua ukiukwaji mkubwa wa  haki za binadamu unaofanyika nchini humo. Hivi karibuni Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump ambaye aliyekuwa akihutubia Bunge la Kongresi la nchi hiyo aliweka wazi uhalisia uliofichika katika siasa za Marekani. Trump alijikita katika kuzungumzia migogoro mikubwa ya kijamii, kiuchumi na tofauti kubwa ya kitabaka kati ya walio nacho na wasiokuwa nacho nchini Marekani na kusema kuwa, uwepo wa watu milioni 49 wasio na ajira, kusambaratika viwanda elfu 60, uwepo wa watu milioni 43 wanaosumbuiwa na njaa, kuchaa kwa miundombinu, uwepo wa magenge ya uhalifu yanayofanya magendo ya dawa za kulevya na hatimaye kuenea ukatili na chuki nchini humo ni kati ya jinai zinazoshuhudiwa sana dhidi ya haki za raia.
Ukandamizaji wa polisi wa Marekani dhidi ya raia
Uchina kama nchi inayoongozwa na mfumo wa chama kimoja kwa zaidi ya miongo sita sasa inaonekana katika fikra za walio wengi kama nchi yenye aina fulani ya udikteta wa kisiasa,. Hata hiyo ukweli ni kwamba, baada ya Vita vya Pili vya Dunia Marekani iliimarisha nafasi yake kwa kutumia taasisi kama vile NATO, Benki ya Dunia na Mfumo wa Fedha wa Kimataifa (IMF). Marekani imezivamia zaidi ya nchi 60 za dunia, kupindu na kuondoa madarakani makumi ya serikali huru, kuanzisha kambi 800 za kijeshi katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa gharama sawa na asilimia 35 ya bajeti yote ya kijeshi ya dunia, mambo ambayo yanaidhihirishia dunia kuwa nchi hiyo ndiye msababishaji wa migogoro ulimwenguni. Jambo lisilo na shaka ni kuwa Donald Trump hatofautiani na marais waliomtangulia wa Marekani.
Mateso yaliyopigwa marufuku na UN yangali yanafanywa na askari wa Marekani dhidi ya watuhumiwa
Uchina inaamini kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imekuwa ikipotosha fikra za walio wengi kuhusiana na suala zima la utetezi wa demokrasia na haki za binaadamu duniani. Uvamizi wa kijeshi wa nchi hiyo huko Iraq na Afghanistan, unabainisha wazi sera za kindumakuwili na hadaa nyingi za Washington kwa walimwengu. Kadhalika sera za kuingilia mambo ya nchi nyingine zinazotekelezwa na Marekani huko katika nchi za Amerika ya Latini ni kati ya hatua nyingine za watawala wa Washington kwa lengo la kutaka kuziondoa madarakani serikali huru za mataifa hayo. Swali la msingi ni kwamba, kwa kuwa na historia hii, Marekani inaweza kuwa na ustahiki wowote wa kuongoza dunia?
Polisi wa Marekani akimuadhibu kwa mateke mwanamke asiye na silaha wala ulinzi
Je kwa mazingira uharibifu mkubwa wa Marekani katika uwanja wa kukiuka haki za binadamu za mamilioni ya watu duniani wakiwemo hata raia wake yenyewe, Washington inaweza kuwa mtetezi wa aki hizo na kuwa mwamuzi na msimamizi wa masuala ya haki za binadamu duniani?
Ni kwa kuzingatia hayo yote ndio maana China ikaitaka Marekani, badala ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, ishughulikie kwanza tatizo la ukosefu makazi la mamilioni ya Wamarekani, kuongezeka raia wa nchi hiyo wanaokabiliwa na njaa sambamba na kukosa huduma muhimu za kimaisha. China inaamini kuwa suala la haki za binadamu linatumiwa na Marekani kama wenzo na fimbo ya kuhalalisha sera za serikali ya Washington za kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine duniani.

0 comments: