Binti Matola alitenga chumba kimoja nyumbani kwake kama Maficho ya Mwalimu Nyerere.
Mzee Sinkala alisema,..."nakumbuka mwaka fulani Serikali ya Kikoloni kupitia Askari wake waliivamia nyumba hiyo nyakati za usiku ili wamuangamize lakini walishindwa kwani Binti Matola alimkimbiza Mwalimu Nyerere kwa kumtorosha kupitia njia ya uani hivyo kufanikiwa kunusuru maisha yake".
Kutokana na Uimara wa Binti Matola kama nguli wa Siasa za Ukumbozi na kama mwanamke shupavu alihudumu Kama kiongozi mwandamizi wa TANU Mkoa wa Mbeya na hii ndiyo ilifanya Mji huo kukua kwa kasi na kutokana na maendeleo hayo ya kiuchumi ilipelekea wanajamii kwenda mitaa hiyo kupata mahitaji mbalimbali kwa kuiita "Soko Matola".
Mzee Sinkala alimalizia kwa kusema pia nyakati hizo Viongozi wa TANU walijenga Jukwaa la Mikutano maalum ya Chama hasa kipindi Hayati Mwalimu Nyerere ajapo ndipo alikuwa akipatumia kuhutubia.
Jukwaa hilo lipo ulipo Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa ,ndani ya Kata ya Maendeleo (Soko Matola)Jijini Mbeya ,maarufu kama "Jukwaa la Mwalimu Nyerere"
Wajumbe wa Kamati ya Utalii Jijini Mbeya wakimsikiliza kwa makini Meya mstaafu wa Halmashauri ya Mbeya Mjini Mzee Sinkala ndani ya nyumba ya kihistoria ya Binti Matola |
Mzee Sinkala akibadilishana mawazo na kijana Thobias Omega, Mjumbe wa Kamati ya Utalii na MwanaHabari kutoka Thobias Omega Blog. |
Hili ndilo Jukwaa la Kihistoria lililojengwa toka enzi za Serikali ya Kukoloni na lilikuwa likitumiwa zaidi na Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere liitwalo "Jukwaa la Nyerere" nje kidogo ya Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa, Jijini Mbeya |
0 comments: