ISRAEL IMEWATIA NGUVUNI WAPALESTINA 420 MWEZI FEBRUARI

Ripoti mpya zinaonyesha kuwa askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewatia nguvuni na kuwaweka kizuizini Wapalestina 420 katika kipindi cha mwezi mmoja tu uliopita wa Februari ukiwa ni muendelezo wa ukandamizaji unaofanywa na utawala huo katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Palestina.
Kituo cha mitaala kuhusu mateka wa Kipalestina kimetangaza katika ripoti yake ya kila mwezi kuwa mahabusu hao wanajumuisha watoto 70 na wanawake 22.
Kituo hicho aidha kimeripoti kuwa Wapalestina wengine 12 wametiwa nguvuni katika eneo lililozingirwa la Ukanda wa Gaza.
Askari wa Israel wanafanya kila aina ya jinai ikiwemo mauaji dhidi ya Wapalestina 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika mwezi uliopita wa Februari mahakama za Israel zimetoa amri 88 za utiaji nguvuni wa kiidara unaoruhusu kuwaweka kizuizini Wapalestina kwa muda hadi wa miezi sita pasina kuwafungulia mashtaka.
Ripoti zinaonyesha kuwa hivi sasa kuna Wapalestina zaidi ya 6,500 wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel…/

0 comments: