BASI LA ALLY'S STAR LAGONGANA NA LORI LA AZAM MISUNGWI MWANZA


Basi la ALLY'S STAR GULF AIR lenye namba za usajiri 514 ANW likitoka Mwanza kwenda Tabora, limepata ajali asubuhi ya leo majira saa moja katika kijiji cha MWAZENZE wilayani Misungwi Mwanza mara baada ya kugongana uso kwa uso na lori la mizigo na kuacha njia.
Kwa mujibu wa maelezo ya abiria waliokuwa wamepanda kwenye basi hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva alipokuwa akijaribu kuovateki gari iliyokuwa mbele yake pasipokujua mbele yake zaidi kuna nini, ndipo basi hilo likagongana ghafla na lori la AZAM lililokuwa limebeba unga wa ngano.
Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyefariki wala kuumia zaidi ya mtu mmoja kupata mshituko wa mguu. Dereva alitoweka mara tu baada ya ajali hiyo kutokea.
(PICHA NA MASENGWA BLOG BLOG)
Lori la mizigo lililogongana na basi hilo likiwa limeharibika baada ya ajali

0 comments: