BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA KIGAMBONI LIMEPITISHA BAJETI YA MWAKA 2017-2018 YENYE VIPAUMBELE MBALIMBALI KWA MASLAHI YA WANANCHI WA WILAYA HIYO

Akivitaja vipaumbele hivyo Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo ya Kigamboni Maabadi Suleiman Hoja amesema bajeti hiyo itajikita zaidi kwenye kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka bilioni 2 mpaka bilioni 8, halikadhalika kuimarisha huduma za afya kwa kuongeza vifaa tiba, kupanua Zahanati, kuboresha huduma za maji, kuboresha masoko na maeneo ya wafanyabiashara, kuboresha sekta ya elimu kwa kuongeza madarasa, nyumba za walimu na kurekebisha matundu ya vyoo, pia usafi wa mazingira wilaya hiyo utakuwa moja ya vipaumbele kwenye bajeti hiyo.
Mstahiki Meya Hoja ameongeza kuwa wanataraji kupokea bilioni 49 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo ruzuku ya serikali, mapato ya ndani, wafadhili na wananchi ambapo amesisitiza kuwa ilikufikia malengo wanatakiwa watumie fursa zilizopo vizuri na kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato.

0 comments: