BARAZA LA KIKAO CHA 17 LA WAFANYAKAZI HOSPITALI YA TAIFA (MNH) LAKUTANA LEO

 Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyaka na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo Dar es Salaam leo
 Baadhi ya Wajumbe na Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa baraza hilo leo.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa baraza hilo leo.
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Margerate  Mrina akitoa mada kwenye mkutano wa Baraza la wafanyakazi ambao umefanyika leo.
 Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Gerald Jeremiah akiuliza swali kwenye mkutano huo leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk. Julieth Magandi, Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Mary Charles  na Mkuu wa Idara ya TEHAMA, Patrick Muro wakifuatilia mkutano huo leo.
 Mwakilishi wa Idara ya Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Primus Saidia akiuliza swali katika mkutano huo leo.
 Wafanyakazi wa hospitali hiyo na baadhi ya wajumbe 
   Mkurugenzi Msaidizi- Elimu na Ushirikishwaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Andrew Mwalwisi akitoa mada leo kwenye mkutano huo leo.
Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo limekutana katika kikao cha 17 pamoja na mambo mengine wajumbe wa baraza hilo wametakiwa kutoa maoni na michango kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.
Akitoa mada katika kikao hicho Mkurugenzi msaidizi –Elimu na ushirkishwaji  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Andrew Mwalwisi amewataka wajumbe wa baraza hilo kuhakikisha wanatoa mrejesho wa vikao vya baraza kwa wafanyakazi kwa sababu yanayojadiliwa ni kwa maslahi ya watumishi wote wa Muhimbili.
“Wale wenzenu mkawaeleze tunayoyazungumza hapa, hivyo ni vizuri mkawaeleze michango mbalimbali inayotolewa kwenye mkutano huu kwani na wenyewe wanatakiwa kufahamu ambacho kimejadiliwa katika kikao hiki,” amesema Mwalwisi.
Agenda zilizopokelewa na kujadiliwa ni mafanikio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/16 na robo mwaka 2016/2017. Pia, Baraza limepokea na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka fedha 2017/2018.
Kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza la wafanyakazi, wajumbe wamemchagua Eneza Somolon Msuya kuwa katibu wa baraza hilo, huku Merina Rwechungura akiwa Katibu Msaidizi.

0 comments: