VIONGOZI WA SOKA DUNIANI KUKUTANA AFRIKA KUSINI

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Duniani FIFA Gianni Infantino juma hili anatarajiwa kukutana na marais wa vyama vya soka zaidi ya 50 katika mkutano wao wa kilele usio wa kawaida nchini Afrika Kusini. Kila taifa mwanachama wa FIFA miongoni mwa mataifa 54 ya muungano huo limealikwa katika mkutano mkubwa mjini Johannesburg, lengo likiwa kujadili masuala muhimu katika mchezo huo na kutolea ufafanuzi mipango ya FIFA kutanua wigo wa Kombe la Dunia na kubadili muundo wa mpango wa maendeleo. Waandaaji wa mkutano huo wamesema marais hao wa vyama vya soka wamegawanywa katika makundi mawili ya watu 25 ambapo la kwanza litakutana na rais wa shirikisho hilo wa dunia Jumanne na lingine siku inayofuata. Huo ni mkutano wa kwanza kabisa wa aina yake wa kilele kufanywa na FIFA ambao unawakutanisha moja kwa moja viongozi wote wa vyama vya soka.

0 comments: