UJERUMANI YARUDISHA MAKWAO WAHAMIAJI 80,000

Ujerumani imewarudisha makwao wahamaji 80,000 ambao maombi yao ya hifadhi yalikataliwa mwaka uliopita na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa mwaka huu wa 2017. Habari hiyo imetolewa na afisa wa ngazi za juu wa Kansela Angela Merkel katika kipindi hiki ambacho kiongozi huyo wa Ujerumani akipigania kuvutia tena hisia za wapiga kura wa chama cha wahafidhina kabla ya uchaguzi wa Septemba. Peter Altmaier, mkuu wa watumishi katika ofisi ya Merkel, ameliambia gazeti la kila Jumapili la Ujerumani la "Bild am Sonntag" kwamba karibu maombi 700,000 ya hifadhi kwa mwaka 2016 yamekataliwa, na kuonesha ishara rekodi nyingine kubwa ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji kwa mwaka huu. Katika lengo la kupunguza tofauti yake na wahafidhinia ilitokana na kufungua mipaka na kuruhusu wakimbizi 2015 Merkel, kiongozi huyo wa chama cha CDU amekuwa katika jitihada za kuwarejesha makwao wakimbizi ambao maombi yao yamekataliwa au wageni ambao wameshiriki vitendo vya kihalifu.

0 comments: