TRUMP ATAFAKARI KUWASILISHA AMRI MPYA YA USAFIRI MAREKANI

Rais wa Marekani Donald Trump, anawazia kutoa amri nyingine mpya ya kuwazuia raia kutoka baadhi ya nchi kuingia Marekani. Hii ni baada ya amri aliyoitia saini kuzuiliwa na mahakama. Trump ametangaza kuwa kuna uwezekeno wa amri nyingine mpya kutolewa siku ya Jumatatu au Jumanne wiki ijayo ambayo haitowajumuisha wenye kumiliki kadi za kijani maarufu kama 'green card' au wakaazi wa kudumu. Mkuu wa utumishi wa umma katika Ikulu ya White House Reince Priebus aliwaambia wanahabari hapo jana kuwa, kuiwasilisha kesi katika mahakama ya juu ni njia nyingine wanayoweza kufikiria katika kutafuta utekelezwaji wa amri hiyo, ambayo iliwapiga marufuku raia kutoka nchi 7 za Kiislamu kuingia Marekani.

0 comments: