TAARIFA YA HABARI TOKA DW, BOMU LAUA 12 AFGHANISTAN IKIWAMO WATOTO

Umoja wa Mataifa umelaani vifo vya raia 12 wa Afghanistan, ikiwa ni pamoja na watoto wanane waliokuwa wakielekea majumbani mwao wakitokea shule, baada ya kulipuka kwa bomu pembezoni mwa barabara. Ni tukio la hivi karibuni katika mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya raia. Shambulio hilo limetokea jana katika mkoa wa Paktika, baadaya ya gari iliyokuwa imewabeba abiria hao kukanyaga bomu ambalo lilitegwa pembezoni mwa barabara. Pernille Kardel, naibu mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amesema watoto kwa mara nyengine tena wanaathirika na mashambulizi ya kiholela ambayo ni kinyume na sheria. Katika ripoti yake ya mwezi uliopita, Umoja wa Mataifa umesema mauaji ya raia yalikuwa ni ya kiwango kikubwa mwaka jana nchini Afghanistan na zaidi ya watoto 3,500 ni miongoni mwa walioathirika.

0 comments: