RC MAKONDA AWATAJA VIGOGO HAWA WAKITUHUMIWA KUJIHUSISHA NA MADAWA...WAPO GWAJIMA, MBOWE,MANJI NA IDDI AZAN

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametaja jumla ya majina 65 wanaotakiwa kufika kituo kikuu cha polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwaajili ya mahojiano.Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari ofisini kwake asubuhi hii, Makonda alisema hiyo ni awamu ya pili baada ya majina ya awali yaliyowahusisha wasanii na askari polisi kuitwa polisi kwa ajili ya kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali.Baadhi ya majina ya washukiwa hapo wanaotakiwa kuripoti polisi Februari 10 ni pamoja na Mbunge wa Hai, Freemani Mbowe, Mchungaji Josephat Gwajima na aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan.Wengine ni Mmiliki wa Slipway, Yach Club, Mwinyi Machata, mmiliki wa Seacliff Casino, Husein Pambakali, wamiliki wote wa Casino, Kiiza, Chizega na wengineo.

0 comments: