PAPAFRANCIS: MACHAFUKO NA UKATILI UKOMESHWE NCHINI KONGO DR
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:19 AM
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ametaka kuhitimishwa machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Papa Francis aliyasema hayo jana Jumapili ambapo sanjari na
kulaani kutumikishwa watoto kama askari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo, amewataka viongozi wa serikali ya Kinshasa kufanya haraka kwa
ajili ya kuhitimisha vitendo vya ukatili nchini.
Katika shambulizi la hivi karibuni la wanachama wa kundi la kigaidi
katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, kwa akali watu 25 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa pia limepasisha azimio la kutaka
kuyanyang'anya silaha makundi ya wabeba silaha nchini humo.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hususan maeneo ya mashariki mwa nchi
hiyo yamekuwa yakishuhudia hali ya mchafukoge kwa zaidi ya miaka 20
sasa kutokana na hujuma za makundi ya wabeba silaha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: