MTOTO LATIFA ALIYEIBIWA SAA 2 ASUBUHI IRINGA MJINI APATIKANA USIKU KIJIJI CHA MKUNGUGU

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwa amembeba mtoto huyo.
Jana mida ya saa 2 asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi aliibiwa mtoto mchanga mweneye umri wa miezi 5. Mtoto huyo aliibiwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi.

Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema ” nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza , baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toaka asubuhi mpaka sasa usiku hatuja muona” .

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh, Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini.

Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtoto huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mwizi huyo wa mtoto. Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh, Ritha Mlagala.

Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh, Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla “pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusio wajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu” alisisitiza

Mkuu wa wilaya. Pichani anaonekana mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi. Picha zingine ni za eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto usiku wa saa 3.

0 comments: