MLIPUKO WAUWA18 SOMALIA

Takribani watu 18 wameuwawa baada ya gari ilililokuwa na viripuzi kuripuka karibu na eneo lenye pirikaprika nyingi mjini Mogadishu, Somalia. Afisa mwandamizi katika eneo la tukio Mohamed Jilibey alithibitisha kuhesabu maiti za idadi hiyo ya watu na kuongeza kuwa watu wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa. Mripuko huo unahesabiwa kuwa wa kwanza mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Somalia tangu kufanyika uchaguzi uliomwingiza madarakani rais Mohamed Abdullahi Mohamed anayetambulika pia kwa jina la Farmajo. Shambulio hilo linaziweka wazi changamoto anazokabiliana nazo rais huyo mpya, ambae amerithi utawala wenye udhibiti mchache wa ardhi ya Somalia kutokana na uwepo wa kundi la al Shabaab. Majeshi ya Umoja wa Afrika yalifanikiwa kuliondosha kundi hilo katika viunga vya jiji la Mogadishu August 2011 lakini wanamgambo wake wameendelea kuyadhibiti maeneo ya vijijini na kurejea mara kwa mara kufanya mashambulizi katika maeneo ya mji huo mkuu wa Somalia.

0 comments: