MLIPUKO WA BOMU WAUA WATU 51 KATIKA ENEO LA AL-BAB, SYRIA

Mlipuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari leo limewauwa karibu watu 51 katika mji wa kaskazini mwa Syria al-Bab. Shambulizi hilo limekuja siku moja tu baada ya operesheni ya kijeshi ikiongozwa na Uturuki kulikomboa eneo hilo kutoka kwa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu. Mlipuaji wa kujitoa mhanga alilipua gari nje ya kituo kimoja cha waasi wa Syria katika eneo la Suesian, kaskazini ya mji wa al-Bad. Hayo yanajiri wakati pande zinazozana katika mgogoro wa Syria zikishiriki mazungumzo ya kutafuta amani yanayoandaliwa jijini Geneva, Uswisi chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Syria Steffan de Mistura anafanya mikutano ya pande mbili na wajumbe ili kuweka mpango wa kutumiwa katika duru hii ya mazungumzo ambayo huenda yakaendelea hadi mapema mwezi Machi.

0 comments: