Akizungumza
mara baada ya makabidhiano hayo eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni
Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate, Mohamed Igbal alisema wameamua kumkabidhi eneo hilo ili kuunga mkono
jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda na kuwakomboa
wananchi wenye uchumi wa kati.
Kwa
upande wake RC, Makonda ameeleza kuwa dhamira ya viwanda ya Rais
Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo, hivyo eneo hilo litatumika kwa
ajili ya ufugaji, kilimo, usindikaji, utengenezaji wa sabuni na eneo
hilo litatumika na wilaya zote.
RC Makonda, alisema mkoa wa Dar es Salaam unajengwa na wana Dar es Salaam
wenyewe hivyo kama kuna watu wanataka kujitolea kwa ajili ya maendeleo
ya Dar es Salaam wafanye hivyo.
0 comments: