MFALME WA SAUDIA KUTUMIA MAMILIONI YA DOLA KUSTAREHE INDONESIA

Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia anatazamiwa kuelekea Indonesia mapema mwezi Machi kwa ajili ya safari ya starehe na anasa itakayogharimu mamilioni ya dola.
Katibu wa Baraza la Mawaziri la Indoneosa Pramono Anung amesema kuwa, Mfalme Salman atawasili nchini humo kuanzia Machi Mosi na kuondoa Machi tisa akiwa ameandamana na watu 1,500.  Siku sita za safari hiyo zitajumuisha safari ya kistarehe katika mji wa kitalii wa Bali ambapo yeye na ujumbe wake wamechukua hoteli kadhaa mjini humo. Maafisa wa Saudia hawajatoa tamko lolote kuhusu safari hiyo ya kistarehe. Mwaka jana Mfalme Salman alitembelea Uturuki ambapo vyombo vya habari vya nchi hiyo vilisema maandalizi ya safari hiyo yaligharimu dola milioni 10 na safari yenyewe iligharimu dola milioni 18. Mfalme huyo alifanya safari kama hiyo nchini Misri ambayo pia iligharimu mamlioni ya dola.
Umasikini Saudi Arabia
Hayo yanajiri wakati ambao Mfalme Salman amekiri kuwa Saudi Arabia inakumbwa na matatizo mengi ya kiuchumi kutokana na kuporomoka bei ya mafuta duniani na pia hujuma ya kinyama ya nchi hiyo dhidi ya Yemen kwa muda wa miaka miwili sasa. Raia wa Saudia wamekatiwa  ruzuku huku bei ya maji, mafuta na umeme ikiongezeka katika jitihada za ufalme huo kubana matumizi.

0 comments: