Polisi wanaoshughulikia masuala ya wahamiaji
nchini Marekani walianzisha opereseheni ya kushtukiza kuanzia siku ya
Jumatatu hadi jana Ijumaa na kuwatia mbaroni mamia ya wahamiaji katika
majimbo sita ya nchi hiyo.
Shirika la habari la Mehr
limeripoti habari hiyo na kusema kuwa, hatua hiyo ya polisi wa Marekani
imechukuliwa ikiwa ni kutekeleza amri wa Rais Donald Trump aliyoitoa
tarehe 27 Januari mwaka huu ya kutaka kufuatiliwa kisheria mamilioni ya
wahamiaji waishio nchini Marekani.
Polisi wa Marekani wanadai kuwa, lengo
la operesheni hiyo ni kukabiliana na wahamiaji wahalifu, lakini
operesheni hiyo inawajumuisha hata wahamiaji ambayo hawana historia
yoyote ya kufanya uhalifu.
Ajenda kuu ya Rais Donald Trump wa Marekani ni kuwafukuza karibu wahamiaji milioni tatu waishio nchini humo.
Majimbo yasiyopungua sita ya Marekani
yameshuhudia uvamizi wa polisi dhidi ya wahamiaji na miongoni mwa miji
kulikofanyika operesheni hiyo ni Chicago, New York na Los Angels. Katika
majimbo ya Carolina Kaskazini na Carolina Kusini nako kumefanyika
operesheni hiyo kali ya kuwatia mbaroni wahamiaji.
Amri ya tarehe 27 Januari ya Donald
Trump iliweka vikwazo vingi pia dhidi ya wahamiaji kutoka nchi saba za
Waislamu za Iran, Iraq, Sudan, Somalia, Libya, Syria na Yemen. Hata
hivyo hatua hiyo imekumbwa na malalamiko makubwa ndani na nje ya
Marekani kutokana na kwenda kinyume na hata katiba ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: