MAJALIWA AFANYA ZIARA BABATI NA MBULU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kulia) akitazama sukari na nishati ya kuni inayotengenezwa kwa kutumia makapi ya miwa inayokamuliwa katika kiwanda cha sukari cha Manyara wakati alipotembelea kiwanda hicho jana Februari 19 2017. Kuni hizo zina ubora unaofanana na ule wa makaa ya mawe na hutumika zaidi katika mitambo inayotumia nishati ya kuni. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na wa nne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa wilaya mstaafa, Mama Sanka baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara mjini Babati akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 19, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) akitazama sanamu ya binadamu wakati alipotembelea moja ya darasa la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo . 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa kwanza kulia) akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wahatzabe wakati alipowasili kwenye hospitali ya Haydom kuanza ziara ya wilaya ya Mbulu.

0 comments: