KESI SABA ZA MAUAJI ZASIKILIZWA MKOANI KIGOMA LEO



Jaji  Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Tabora Sam Rumanyika  akikagua  Kikosi cha Kutuliza ghasia  FFU wakiwa  katika gwaride la kumpokea mkoanio kigoma kabla ya kusikiliza kesi saba za mauwaji zilizosikizwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya kigoma hapo leo (PICHA NA MAGRETH MAGOSSO). 
NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

JUMLA ya Mashauri saba ya kesi za mauaji yameanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Kigoma mkoani  hapa  na Jaji mfawidhi  mahakama kuu Kanda ya Tabora  Sam Rumanyika kwa lengo la  kuongeza ufanisi na kuwapunguzia gharama wateja wao.

Akitoa kauli  hiyo  leo kwenye viwanja vya mahakama hiyo katika ufunguzi wa usikilizwaji  wa kesi hizo, Naibu Msajili  Mahakama kanda  ya tabora Shamillah Sarwatt alisema wanafanya kazi ya kusikiliza mashauri  ya kesi za mauaji ndani ya  muda katika maeneo husika ili, kutoa  haki kwa wateja.

Alifafanua kuwa, kazi ya mahakama ni kusikiliza mashauri na kutoa haki kwa wote na kwa wakati hasa katika shauri la mauaji  nia kumwezesha mteja asitumie gharama kubwa kutafuta haki hizo, ambapo serikali imejiwekea utaratibu huo, ili kuongeza ufanisi kwa wadau wa idara ya sheria.

Alieleza kuwa, miongoni mwa mashauri ya mauaji hayo awali  zilishasikilizwa katika vipindi tofauti tofauti hususani mashauri ya mwaka 2007 na mwaka 2012 ambapo zilishafikishwa katika mahakama ya rufani hali inayoilazimu mahakama ya kanda kuwafuata wateja maeneo husika ili kutoa haki kwa wote.

Alianisha kuwa kesi tano zitasikilizwa leo katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya kigoma na mashauri mawili yatasikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Kibondo ambapo wateja watatumia fursa hiyo katika kupata haki zao za msingi kabla ya kutolewa hukumu husika.

Awali  kabla ya kusikilizwa ka mashauri hayo Jaji  Sam Rumanyika alikagua gwaride la Kikosi cha Askari wa kutuliza ghasia( FFU) hatimaye mchakato wa usikilizaji wa kesi tano za mauwaji dhidi ya walengwa zilianzwa kusikilizwa .

0 comments: