DIWANI AWAFIKISHA MAHAKAMANI MWENYEKITI NA MTENDAJI WA KIJIJI KAZULAMIMBA-KIGOMA





NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

DIWANI wa Kata ya Kazulamimba  wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma, Nuru Shakali amesimamia zoezi la kuwafikisha Mahakamani Mwenyekiti wa kijiji cha Kazulamimba Juma Kibuye na Ofisa Mtendaji  Abduli Mwinga kwa  tuhuma za wizi wa matofali na mchanga  wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho kinyume cha sheria, kanuni na taratibu husika.
                                                        
Pia huwakata fedha kiasi cha sh.10,000 wanufaika wote wa Mradi wa Tasaf bila maelezo sahihi ya matumizi ya  fedha hizo, hali inayowapa wakati mgumu wanufaika kwa kuwa hawapewi hata risiti yenye kuonyesha uwajibikaji wa kukatwa kwa fedha hizo kinyume cha sheria na taratibu za mfuko huo.

                                                       
Hayo yamebainika juzi katika kijiji hicho ambapo diwani akiongozana na Askari polisi wa katani humo kwa ajili ya hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa hao,ambao wamehujumu mradi wa wananchi kwa kuuza  kinyemela ,tofali na mchanga  wenye thamani ya zaidi ya milioni 2 ,bila ridhaa ya umma.

Akithibitisha hilo Nuru Shakali alieleza kuwa,alipokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na Februari,16,2,2017 alibaini uhalisia wa wizi huo baada ya mkandarasi wa zahanati hiyo kuanisha kila hatua ya uzwaji wa tofali 9,700 sanjari na tripu 11 za mchanga ambazo zina thamani ya zaidi ya fedha milioni 2.

Alisema  amebaini uzozo mkubwa katika serikali ya kijiji hicho kwa uda mrefu lakini amechoshwa na hulka zao,ambazo zitachangia wananchi washindwe kuchangia nguvu zao katika miradi ijayo hali iliyomlazimu kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine hasa wapiga dili.

Kwa nyakati tofauti  wenyeviti wa kitongoji cha kilelema A na C  wa kata hiyo Jacksoni Biaga na Ramadhan Haruna walisema  tuhuma zinazowakabili viongozi hao ni kweli kwa kuwa katika kikao kilichoketi 15, februari,2017 walikiri kwa mandishi juu ya ubadhilifu wa mali za umma.

Waliongeza kuwa,awali viongozi hao waliwashawishi wenyeviti wa vitongoji hivyo kuwa,wauze tofali na mchanga kinyemela ,hali ambayo walikataa wakiwataka waitishe kikao cha umma kama wanahitaji kufanya hivyo,lakini walitumia nyadhifa zao kuuza mali za wananchi kinyume cha sheria,kanuni na taratibu.

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho Gervas Kengwa na Casian Mabondo kwa nyakati tofauti wakiri wananchi kutoka vitongoji sita walichangia nguvu ya mchanga,tofali kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya awali na mradi mpya wa zahanati ya kisasa lakini walishangaa viongozi kuuza kinyemela ilihali kuna kero ya ukosefu wa zahanati bora.

0 comments: