DCB YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA DROO YA PILI YA WEKA NA AMANA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WASHINDI wa bahati nasibu ya kampeni ya kuweka amana DCB inayojulikana kama Boresha maisha na DCB wamekabidhiwa zawadi zao  na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima leo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza kabla ya kutoa zawadi kwa washindi hao, Kpilima amesema kuwa hii ni droo ya pili ya bahati nasibu kwa wateja wa benki hiyo kunufaika na kampeni ya kuweka amana kwa akaunti za Akiba binafsi, akaunti za watoto na WAHI iliyoanza mwezi Novemba mwaka jana.

Kapilima amesema kuwa, lengo kuu la kampeni hii ni kuboresha maisha ya wateja wa benki hiyo kwa kuwapatia zawadi mbalimbali pindi mteja anapokuwa anaweka fedha mara kwa mara na inawadsaidia kuongeza ukubwa wa amana na kuwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba benki kwa matumizi ,mengine.

Katika droo ya pili iliyochezwa mbele ya mkaguzi kutoka michezo ya bahati nasibu ya Taifa Bakari Maggid iliweza kutoa washindi wawili wa simu za mkononi, washindi wa tatu wa fedha taslimu za ada na washindi ishirini wa tshirt.
  Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima akimkabidhi zawadi ya simu Mercelina Haule wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa bahati nasibu ya  kuweka amana DCB inayojulikana kama Boresha maisha na DCB leo Jijini Dar es salaam.
  Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa ajili ya ada ya watoto, Ziada Haule wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa bahati nasibu ya  kuweka amana DCB inayojulikana kama Boresha maisha na DCB leo Jijini Dar es salaam.
   Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima  akikabidhi zawadi za Tshirt kwa wateja waliofanikiwa kushinda bahati nasibu ya  kuweka amana DCB inayojulikana kama Boresha maisha na DCB leo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washindi wakiwa katika picha ya pamoja na  Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima   (katikati), Meneja mwandamizi wa benki na matawi Haika Machaku(wa kwanza kulia) wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa bahati nasibu ya  kuweka amana DCB inayojulikana kama Boresha maisha na DCB leo Jijini Dar es salaam.

0 comments: