DAKTARI FEKI ATIWA MBARONI KIGOMA UJIJI JANA



NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

MMILIKI Mmoja wa duka la dawa  muhimu kwa binadamu katika eneo la Kibirizi  Manispaa ya Kigoma Ujiji ,ametiwa mbaroni katika kituo cha polisi  central kwa tuhuma za  kuendesha duka  la dawa kama Hospitali huku akitoa huduma mbali mbali ikiwemo kung'oa meno  wagonjwa .

 
Kukamatwa kwa mmiliki huyo ni matokeo ya ukaguzi uliofanywa juzi na timu ya idara ya afya ya Halmashauri ya Manispaa ya kigoma Ujiji ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dkt.Peter Nsanya.


Dkt.Nsanya alisema kuwa katika ukaguzi wao wamegundua kwamba pamoja na kuendesha shughuli mbalimbali zikiwemo za uuzaji wa madawa, kuchoma sindano, kung’oa meno na mambo mengi ya matibabu ya afya ,
huku akijua  hana taaluma ya utabibu na  kibali cha kuendesha shughuli hiyo ambapo ni kinyume cha sheria, kanuni nataratibu za wizara husika.


Akizungumzia tukio hilo Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava amewataka wananchi hao kutumia vituo vya afya na zahanati zilizo rasmi  hasa  za serikali ambazo zinauhakika na utoaji huduma na kulinda afya zao.


Hata hivyo wananchi wa eneo hilo wameeleza kusikitishwa  kwa kitendo cha kukamatwa kwa  mmiliki huyo sanjari na kufungwa kwa duka hilo ambalo  lilikuwa tegemeo lao kubwa katika upataji wa  tiba wenye tija na kwa haraka.


Kwa upande wa Mmiliki wa duka hilo la dawa, Alex Hussein maarufu kama Ndevu alisema  taalumahiyo amepewa na mungu haoni sababu ya kukamatwa kwake kuwa hajaharibu afya za wateja wake.

0 comments: