MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
IMEELEZWA kuwa,
Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Wawachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kupeleka
malalamiko katika kamati ya maadili ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ili kuwakumbusha
wajibu wao, madiwani waliopigana katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma ujiji
katika Kikao cha baraza la madiwaniti hivi karibuni.
Hayo yalisemwa jana
katika ukumbi wa kizoto Manispaa ya Kigoma ujiji katika Kongamano la Wanachama wa ccm wilayani
kigoma Mjini na Viongozi wa Chama katika sherehe ya miaka 40 ya CCM,
alisema Kitendo hicho cha Madiwani kupigana katika jengo la Halmashauri
hakipaswi kufumbiwa macho ni lazima Wachukuliwe hatua za kinidhamu ili iwe
fundisho kwa wengine.
Akithibitisha
hilo Mwenyekiti wa Chama hicho kigoma Dkt, Aman Kabourou alisema kitendo
cha diwani Revocatusi Chipando (BABA REVO) kumtuhumu Diwani wa kata ya Kibirizi Rashid Luhomvya
kwa madai kuwa diwani mwenzake huyo wa
chama hicho ni mwizi wa miradi ya umma,
Alisema
tabia zinazo endelea katika Manispaa hiyo kwa kushirikiana na Viongozi wa halmashauri kuiba fedha za miradi
ya maendeleo kwa kuahidiana kugawana lakini pindi wanapo hindwa kutimiza ahadi zao
wanapigana katika kikao cha madwiani kwa
kuwatumia madiwani wasio na haya akiwemo Baba Revo.
"
Manispaa ni jengo tukufu liheshimiwe na kila mtu, suala la madiwani
kupigana katika halmashauri lichukuliwe hatua za kinidhamu hatuwezi kuvumilia
sisi kama Chama kinacho tawala na Serikali iliyopo madarakani, lazima tuhakikishe
sula hili linashugulikiwa , maendeleo hayaji
madiwani wataendelea na malumbano",alisema Kabourou.
Alisema
Wananchi wa Manispaa ya Kigoma Walifanya Makosa kuikabidhi halmashauri
chama ambacho kinahitaji kujijenga (ACT)
kwa kuwa hakiwezi kushughulikia kero za
wananchi kwa lengo la kuchochea maendeleo na uchaguzi ujao wasirudie
makosa waliyoyafanya leo.
Kwa upande Wake
katibu wa Mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala alisema Suala la CCM kupoteza jimbo la
Kigoma mjini pamoja na kata zote ni usaliti uliofanywa na baadhi ya Wanachama
wa CCM waliokisaliti Chama kwa kupewa rushwa hali inayowatesa raia ambao
walipiga kura kwa njia ya rushwa.
Alisema katika
kuiunda CCM mpya na Serikali mpya watahakikisha wanawaondoa wasaliti wa chama hicho waliopelekea kushindwa katika chaguzi zake na kuonya mamluki
kuwa ccm ndio mtatuzi wa kero za wananchi kwa ujumla.
Aidha
Wanachama kupitia uchaguzi wa viongozi wa
Chama 2017 wahakikishe wanatenda haki kwa kuchagua viongozi wenye sifa
bila kujali masuala ya rushwa yanayo sababisha kuua Chama kwa kuwa, baadhi ya
viongozi wanatumiwa na Vyama vya
upinzani ili,kukiangusha chama hicho.
Alisema wakibaini kiongozi
ameshinda kwa kutoa rushwa watamuondoa , hakuna kiongozi anae shinda kwa misingi
ya rushwa na kukitumikia Chama kwa uzalendo na uadilifu kwa kuwa,wengi wao ndio wale wasariti wa chama wakipewa pesa wako radhi kukiuza
chama na kudai Viongozi wa aina hiyo
hawaitajiki ccm.
Kwa
upande wake katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kigoma mjini Zuberi
Mabiye alisema kitendo cha Diwani wa kata ya Kibirizi Ruhovya Yunusi na diwadi wa kata ya Mwanga Kasikazini
Revocatusi Chipando (Baba Revo ) si cha
ungwana kwa raia na kama wananyimana miradi watumie kamati za huduma za kijamii
kujadili hayo.
0 comments: