BENKI YA UBL KUWEKEZA KATIKA KILIMO NCHINI TANZANIA

UB1
Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), akielezea nia ya Benki yake ya kutaka kuwekeza kartika Sekta ya Kilimo, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) ofisini kwake jijini Dar es salaam. 
UB2
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akichukua maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), baada ya ya Mtendaji huyo kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam na kueleza nia ya kuzitumia fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo.
UB3
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akielezea namna matumizi ya vifaa vya Kielektroniki (EFDs) yalivyoongeza  Makusanyo ya Mapato ya Serikali alipotembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), Ofsini kwake jijini Dar es salaam.
UB4
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akielezea riba nafuu ambayo wananchi wengi hupendelea kutoka katika Benki baada ya  kutembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall, Ofsini kwake jijini Dar es salaam.
UB5
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Kilimo unaotaka kufanywa na Benki ya UBL Nchini Tanzania baada ya kukutana na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Faisal Aliza Jamall OfIsini kwake jijini Dr es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Benki ya ya Uarabuni, UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni na pia kufanya kazi na Watanzania pamoja na Serikali yake.
Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal Jamall wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Bw. Jamall alisema kuwa kwa sasa Tanzania inaenda vizuri hasa katika suala la ukuaji wa uchumi ingawa kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa fedha zimeadimika mitaani lakini ni wazi kwamba Taifa linarudi kwenye utaratibu. Hivyo wameonesha nia ya kuwekeza hasa katika Sekta ya Kilimo.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa hali inabadilika na Jumuiya ya Mabenki inaanza kuwa na imani na Tanzania. Na kuongeza kuwa kitendo cha Benki ya UBL kuonesha nia ya kufanya kazi na Serikali katika Sekta ya Kilimo ni jambo jema katika maendeleo ya haraka ya Tanzania kwa kuwa Sekta hii mama bado inakabiliwa na changamoto nyingi.  
Alisema dhamira kubwa ya Benki ya UBL ni kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo pamoja na uvuvi. Na Serikali imeahidi kuitumia vizuri fursa hii ili nchi iweze kupiga hatua ya haraka zaidi hasa katika kipindi ambacho imedhamiria kuwa nchi ya Viwanda.
Akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya dola katika uchumi badala ya shilingi ya Tanzania, hasa kwenye mikopo, Waziri Mpango alisema kuwa suala hili Serikali imeshaanza kulifanyia kazi kwa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa karibu biashara ya maduka ya fedha za kigeni.  
“Tumepiga hatua ya kufunga mashine za kielektroniki (EFDs) ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuona kinachofanyika ili wamiliki wa maduka hayo walipe kodi inayostahili. Aidha zoezi hili litaweizesha Benki Kuu ya Tanzania – BoT, kuona kiasi cha fedha za kigeni zilizopita katika maduka na itaimarisha matumizi ya shilingi ya Tanzania; japo tuna changamoto kubwa ya wananchi kutokudai risiti pindi wanapopata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni,” Alisisitiza Dkt. Mpango.
Katika kuhitimisha majadiliano hayo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mpango alisema Serikali itaongeza ushirikiano na Benki ya UBL ili waweze kufanya biashara, ikizingatiwa kuwa Benki hiyo ni miongoni mwa Benki kubwa katika nchi za Uarabuni.

0 comments: