AGIZO LA TRUMP LAMKUMBA MWANAMICHEZO WA MAREKANI MWENYE IMANI YA KIISLAMU

Mchezaji wa Marekani wa mchezo wa fencing mwenye Imani ya dini ya Kiislamu, Ibtihaj Muhammad amejikutana akizuiliwa kwa masaa mawili katika kiwanja cha ndege bila kuambiwa sababu ya kuzuiliwa kwake na hata yeye mwenyewe akiwa hajui sababu ya wafanyakazi wa kiwanja hicho kumzuia.Akielezea tukio hilo, alisema amekuwa akisikia tu watu wakiongea kuwa kuna nchi saba zimezuiliwa kuingia Marekani lakini hakuwa akijua zaidi na lakini na yeye imemtokea na anahisi wafanyakazi wa uwanja wa ndege aliotumia walidhani na yeye ni mmoja wa wakimbizi kutoka mataifa yaliyozuiliwa lakini anashangaa kwanini alizuiliwa na hali yakuwa anakila kitu kinachomtambulisha kuwa Mmarekani.
“Wiki kadhaa zilizopita nilizuiliwa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege kwa masaa mawili, sijui kwanini. Siwezi kusema kwanini ilinitokea, lakini najua mimi ni Mwislamu na nina jina la Kiarabu, na hata hivyo naiwakilisha timu ya Marekani na nina vifaa vya Olympic lakini hilo bado halijabadili mwonekano wangu na jinsi watu wanavyonichukulia,” alisema Muhammad.
Kuziliwa kwa Ibtihaj Muhammad kumekuja ikiwa ni sehemu ya agizo la Rais wa Marekani, Donald Trump kuzuia wakimbizi kutoka mataifa saba yenye imani kali ya Kiislamu mpaka watakapoimarisha hali ya usalama na kuwa imara ndipo wataruhusiwa tena kuendelea kuingia nchini humo.
Ibtihaj Muhammad ni Mmarekani wa kwanza mwenye imani ya Kiislamu kushinda medali katika mashindano ya Olimpiki akiwa amevaa hijabu mwanzo mpaka mwisho wa mashindano.

0 comments: