AFISA WAZAMANI WA POLISI ADAI KUTEKELEZA MAUAJI KWA AMRI YA DURTERTE

Afisa wazamani wa Polisi nchini Philipine hii leo amedai kuwa Rais Rodrigo Durterte alimuamuru yeye pamoja na maafisa wengine wa kikosi cha mauaji kuwaua wahalifu na wapinzani wake wakati Duterte alipokuwa meya wa mji wa Davao kusini mwa nchi hiyo. Arthur Lascanas afisa wa zamani wa polisi nchini humo ameeleza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kikosi hicho cha mauaji kilipokea kati ya dola 400 na 100,000 kwa kila mauaji ya mtu mmoja yaliyotekelezwa kwa amri ya Durtete. Afisa huyo amesema aliongoza mauaji hayo dhidi ya watumiaji na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya pamoja na wahalifu wa makosa madogodogo katika mji wa Davao wakati Duterte alipokuwa Meya wa mji huo kwa zaidi ya miongo miwili. Amesema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na mtangazaji anayepinga ukomunisti Jun Pala pamoja na ndugu wawili wa kiume wa afisa huyo na kuwa anakiri kufanya mauaji hayo na anaomba radhi kwa Mungu. Maelezo ya Lascanas yanatofautiana na na ushahidi wake aliotoa awali mbele ya tume ya uchunguzi ambapo alisema mauaji hayo hayakufanyika.

0 comments: