VYOMBO VYA HABARI NCHINI VYATAKIWA KUWA CHACHU YA MABADILIKO KUELEKEA UCHUMI WA KATI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media group wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Mlimani Tv na Redio iliyo chini ya Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru Production inayomiliki vituo vya azam Tv na Redio wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Azam Tv na Redio iliyo chini ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika Kipindi cha Alasiri Lounge kinachorushwa na Azam Tv iliyo chini ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali imevitaka vyombo vya habari nchini kuwa chachu ya mabadiliko katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchumi wa kati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye katika ziara yake kwa vyombo vya habari vya Clouds, Mlimani na Azam, ziara inayolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya Serikali na vyombo vya habari nchini.

“Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika ajenda mbalimbali ikiwemo kutoka katika hali ya uchumi tuliona nao sasa kuelekea uchumi wa kati hivyo vyombo vya habari vinatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha suala hili linawafikia na kuleta uelewa kwa wananchi”alisema Mhe. Nnauye.

Waziri Nape alisisitiza kuwa, kumekuwa na mitazamo tofauti katika vichwa vya wananchi au jamii kwa ujumla kuhusu suala zima la kuelekea uchumi wa kati, hivyo ni jukumu la vyombo vya habari nchini kuweza kuwaelewesha nini maana halisi ya uchumi unaolengwa kuufikiwa.

“tumesikia ya kwamba uchumi wa nchi umekuwa kwa asilimia saba, mwananchi wa kawaida hawezi kuwa na uelewa wa kujua ni vipi uchumi wa nchi unakuwa, hivyo vyombo vya habari vina mchngo mkubwa katika kuifanya jamii kuwa uelewa juu ya ukuaji wa uchumi” alisisitiza waziri Nape.

Mbali na hayo Waziri Nape amesema kuwa vyombo vya habari ni chanzo cha wananchi kuwa kitu kimoja katika kulinda amani ya nchi na utamaduni uliopo, hivyo vina budi kuzidi kutunza utamaduni uliopo pamoja na kuwafanya wananchi kupenda utamaduni wao.

Waziri Nape alisisitiza kuwa vyombo vya habari viifanye jamii kwa ujumla kuwa na utamadumi hasa wa utamaduni wa ulipaji wa kodi katika nyanja tofauti na kuwa wazalendo kwa maendeleo ya nchi.

“sisi kama wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla tunatakiwa kutengeneza vijana ambao kwao kulipa kodi ni fahari, vijana ambao kazi kwao ni heshima pamoja na kutengeneza vijana ambao hujivunia uzalendo wa nchi yao”Alisema Waziri Nape.

Hata hivyo Waziri Nape ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali na vyombo vya habari nchini katika nyanja tofauti ikiwemo utoaji wa habari muhimu za utekelezaji wa Serikali katika kuleta maendeleo nchini.

0 comments: