Senegal iliteuliwa na ECOWAS ili kuongoza operesheni ya kuingilia kijeshi dhidi Rais Yahya Jammeh.
Mkurugenzi
wa Habari na Uhusiano wa Umma wa majeshi ya Senegal (DIRPA) ameiambia
BBC kuwa mipango ya shughuli za kuingilia kijeshi imeanza.
"Jenerali François Ndiaye, Mkuu wa jeshi la ardhini ndiye ataongoza askari wa Senegal," amesema Bw Ndiaye, mkurugenzi wa DIRPA.
Mwandishi
wa habari wa Senegal ambaye anaishi katika mji wa Ziguinchor amesema
kuwa askari wa Senegal wamewasili katika bandari ya Ziguinchor, kusini
mwa Senegal.
Senegal
iliteuliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS)
kuongoza operesheni ya kuingilia kijeshi nchini Gambia kumuondoa
madarakani rais anayemaliza muda wake yahya Jammeh ambaye amekataa
kuachia madaraka baada ya kushindwa Desemba 1.
Aidha,
viongozi tawala katika manispaa ya jiji la Djouloulou katika mkoa huo wa
kusini mwa Senegal, kilomita kumi na tano na mpaka wa Gambia,
amewatolea wito viongozi wa Senegal na mashirika yasiyo ya kiserikali
kusaidia kuwahudumia maelfu ya watu ambao waliikimbia nchi ya Gambia na
katika mji huo.
Kwa
mujibu wa Katibu wa manispaa ya jiji la Diouloulou, Amadou Oury Diallo,
toka kushindwa kwa rais anayemaliza muda wake Yayah Jameh katika
uchaguzi wa urais wa Desemba 1, Djouloulou imewapokea karibu watu 800
ambao wanawasili na kiwango kidogo cha chakula na mavazi.
Wakati
huo huo katikamji wa Banjul hali ya wasiwasi imetanda ikiwa zimesalia tu
saa chache ili kukamilika kwa muda wa kuongoza kwa muhula wa Rais Yahya
Jammeh.
Mitaa imebaki patupu wakati ambapo watalii kutoka mataifa ya mataifa mbalimbali wameondoka nchini humo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: