RAIS MAGUFULI ASEMA SERIKALI YAKE ITASAMBAZA UMEME KILA KIJIJI, ASEMA UMEME HAUTAPANDA BEI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba  Desiderius Rwoma mara baada ya kushiriki Misa ya Mwaka mpya kanisani hapo. Katikati ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.


NA K-VIS BLOG
RAIS John Pombe Magufuli, amewahakikishia Watanzania kuwa, serikali ya awamu ya tano itasambaza umeme kwenye vijiji vyote, tena kwa bei nafuu.
Rais aliyasema hayo leo Januari 1, 2017, wakati wa ibada ya kusherehekea mwaka mpya kwenye kanisa Katoliki jimbo la Bukoba.  
“Tutahakikisha tunasambaza umeme mpaka vijijini ili kila Mtanzania anufaike na huduma hii bila kujali hali yake.” Alisiema Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliwaondoa  hofu Watanzania kuwa bei ya umeme haitapanda licha ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji EWURA, kutangaza ongezeko la bei ya nishati hiyo kwa asilimia 8.5 kuanzania Januari Mosi, 2017.
“Haiwezekani kupandisha bei ya umeme hasa ukiwa na mikakati mikubwa ya kujenga viwanda.” Alisema Dkt. Magufuli wakati akitoa salamu zake mbele ya waumini wa dini ya Kikristo wakati wa ibada hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibusu mkono wa Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Ibada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba  Desiderius Rwoma mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya Ibada.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Marehemu Kadinali Rugambwa mara baada ya Ibada kanisani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na watawa wa kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba mara baada ya Ibada. (PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba  Desiderius Rwoma kushoto pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni Kanisani hapo.

0 comments: