OBAMA AAGA, ASEMA UBAGUZI DHIDI YA WAISLAMU NCHINI MAREKANI HAUKUBALIKI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:29 PM
Rais Barack Obama wa Marekani ametahadharisha kuhusu mwenendo wa kudumishwa mifarakano na ubaguzi katika nchi hiyo.
Obama ambaye alikuwa akitoa hotuba ya kuaga Wamarekani katika
mji wa Chicago baada ya kuiongoza Marekani kwa mihula miwili, amesema
kuwa ubaguzi bado ni nguvu inayozusha mifarakano katika jamii ya
Marekani. Vilevile ametahadharisha kuhusu hali ya kisiasa ya nchi hiyo
na kusema: Ubaguzi wa kizazi ndio tishio kubwa kwa demokrasia ya
Marekani.
Rais Barack Obama amesema ubaguzi unaofanywa dhidi ya Waislamu nchini Marekani haukubaliki.
Katika hotuba yake ya kuwaanga Wamarekani, Obama amesema kuwa
makubaliano ya nyuklia ya kundi la 5+1 na Iran na kuanzisha tena
uhusiano na Cuba ndiyo matunda muhimu zaidi ya kipindi cha utawala wake.
hata hivyo ongezeko la mauaji ya Wamarekani wenye asili ya Afrika na
ukatili wa polisi ya Marekani wa kuwapiga risasi watu weusi ni tishio
kubwa kwa jamii ya Marekani na mambo hayo yanailekeza kuzimu taratibu
jamii ya nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa, Mmarekani mmoja mwenye asili ya Afrika huuliwa
kwa kupigwa risasi na polisi kila baada ya masaa 28 nchini Marekani, na
hicho ndicho kiwango cha juu zaidi cha kuuliwa watu weusi duniani.
Kipindi cha uongozi wa miaka 8 ya Barack Obama kinamalizika wiki ijayo kwa kuapishwa rais mteule wa Marekani Donald Trump.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: