MASWALI YAIBUKA KUHUSU KUJIUA KWA AFISA MWANDAMIZI NCHINI MISRI

media
Akihusishwa katika kesi ya rushwa, afisa mwandamizi wa Misri ajiua  gerezani.
Katibu Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Misri amejiua Jumatatu hii Januari 2, siku moja baada ya kukamatwa kwa uchunguzi kuhusu rushwa, maafisa wa mahakama wamesema.
Shalaby Wael alikamatwa Jumapili alifajiri Januari 1, 2017 kwa kuhojiwa kuhusu kesi ya hongo katika mahakama ya juu ya nchi hiyo.
Kukamatwa kwake kunakuja siku chache baada ya Mamlaka ya Ukaguzi kwa Viongozi, inayohusika na kupambana dhidi ya rushwa katika taasisi za umma, kumkamata afisa wa ununuzi katika Baraza la Kitaifa, Gamal al-Labban.
Maongezi ya simu ya Gamal al-Labban yalionyesha kuwa Chalabi "alihiriki katika mambo kadhaa" yanayoendana na uchunguzi unaoendelea, amesema afisa wa mahakama.

0 comments: