Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye yupo
nchini kwa ziara ya siku 2.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye
ameongozana na ujumbe wake kwa ziara ya siku 2 wengine waliohudhuria ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.
Januari Makamba (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.
Faustine Kamuzora.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari
Makamba akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mkuu wa
UNEP Bw. Erik Solheim na ujumbe wake .
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ameliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuisaidia
Tanzania kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira katika
maeneo mbalimbali nchini ambao umepelekea mamia ya ekari za misitu
kutoweka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na
kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja
wa Mataifa (UNEP) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na Serikali kufanya
jitihada kubwa za kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira
ikiwemo mpango wa upandaji wa miti kote nchini lakini bado msaada na
nguvu zaidi inahitajika kutoka shirika la Mazingira la UNEP ili kuongeza
kasi ya kukabiliana na tatizo hilo nchini.
Amesema
Tanzania ina mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Shirika la UNEP ambapo
shirika hilo limeweza kuisaidia nchi katika miradi mbalimbali ya
kuhifadhi mazingira hivyo mahusiano hayo mazuri ni muhimu yakaja na
mbinu bora na nzuri za kuhifadhi mazingira ili kuokoa Taifa lisigeuke
jangwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini.
Makamu wa
Rais pia amehimiza wataalamu wa mazingira wajikite zaidi katika kutoa
elimu kwa wananchi watumie nishati mbadala kama gesi na makaa ya mawe
ili kudhibiti tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa
miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
ERIC SOLHEIM amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya
kukabiliana na uharibifu wa mazingira na kusisitiza kuwa Shirika hilo
litaendelea kushirikiana na Serikali Tanzania katika Uhifadhi wa
mazingira nchini.
Mkurugenzi
huyo amesema suala la kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira
sio la Serikali pekee hivyo ni muhimu kwa Serikali kushirikiana ipasavyo
na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupambana na tatizo ili kupata
suluhu ya kudumu.
Naye,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January
Makamba amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa UNEP hapa nchini ni fursa ya
kipekee ya kufungua na kuimarisha ukurasa mpya wa mahusiano kati ya
Tanzania na UNEP.
Makamba
amesema kuwa Serikali imetengeneza programu mpya Tano za mazingira
ikiwemo kupunguza matumizi ya mkaa ili kuhifadhi misitu,vyanzo vya
maji,kushughulikia taka na kujenga uwezo kama hatua mpya kabisa ya
kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: