HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI INATOWA HUDUMA YA USHAURI WA LIISHE NA AFYA BURE


  Mtaalamu wa Lishe na Afya Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Maduhu Mashini (kulia) akimpima urefu Muuguzi wa Afya Hospitali hiyo,  Agatha Hiza wakati alipofika  kupata huduma ya Ushauri wa Liishe na Afya inayotolewa bure Hospitalini hapo, ambapo kilele chake itakuwa Feb 3, 2017.

 Mtaalamu wa Lishe na Afya Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Maduhu Mashini (kulia) akiweka sawa kifaa 
 Mtaalamu wa Lishe na Afya Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Maduhu Mashini (kulia) akimwelekeza Muuguzi wa Hospitali hiyo kifaa kinachotumika kupima uzito pamoja na kukokotoa uwiano kati ya uzito na urefu, mafuta ya mwili na mafuta yanayozunguka ogani kuu mwilini kama moyo, ini na figo, ambapo huduma hizo zinapatikana bila malipo yoyote. huduma zinapatikana Jengo la Magonjwa ya nje  (N O P D) sehemu ya kusubiria ndugu wa wagonjwa.
   Mtaalamu wa Lishe na Afya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Denis Mbinga (kushoto) akimwelekeza jambo Dereva wa kujiajiri, Mussa Kitinga  kifaa jinsikinavyofanya kazi katika kupima uzito pamoja na kukokotoa uwiano kati ya uzito na urefu, mafuta ya mwili na mafuta yanayozunguka ogani kuu mwilini kama moyo, ini na figo, ambapo huduma hizo zinapatikana bila malipo yoyote. huduma zinapatikana Jengo la Magonjwa ya nje  (N O P D) sehemu ya kusubiria ndugu wa wagonjwa.
Mtaalamu wa Liishe na Afya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Elizabeth Lyimo akimwelekeza jambo,  Seifu Ramadhani wakati wa upimaji Afya ukiendelea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ukiendelea hadi Feb 3, 2017.

0 comments: