BARAZA LA USALAMA LA UN LATHIBITISHA IRAN IMETEKELEZA MAKUBALIANO YA JCPOA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza katika kikao chake kilichofanyika usiku wa kuamkia leo kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza majukumu yake yote kuhusu makubaliano ya nyuklia kati ya Tehran na kundi la 5+1 maarufu kwa kifupi kama JCPOA.
Mwakilishi wa Ulaya katika kikao cha jana cha Baraza la Usalama kilichofanyika kuchunguza jinsi Iran ilivyotekeleza makubaliano ya JCPOA, amesema kuwa Baraza la Usalama litapokea tena ripoti kuhusu faili hilo miezi sita ijayo. Afisa huyo wa Umoja wa Ulaya amemnukuu Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja huo Bi Federica Mogherini akisema kuwa, makubaliano ya nyuklia ya Iran sasa ni makubaliano ya kimataifa. 
Kwa upande wake mwakilishi wa Ufaransa amesema katika kikao hicho cha UN kwamba, uhusiano wa nchi yake na Iran umeboreka baada ya makubaliano ya JCPOA. Mjumbe wa Uingereza ambaye pia amehutubia kikao hicho amesema ulimwengu uko tayari kushirikiana zaidi na Iran katika masuala ya kiuchumi.
Baraza la Usalama la UN
Hata hivyo kauli ya Umoja wa Mataifa kwamba Iran imetekeleza kikamilifu majukumu yake kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hayakuifurahisha Marekani. Mwakilishi wa serikali ya Washington katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power ameendeleza uhasama wa miaka mingi wa Marekani dhidi ya Iran na kusema kuwa, makubaliano ya JCPOA hayapasi kulifanya Baraza la Usalama lisizingatie masuala mengine ya Iran.
Samantha Power
Samantha Power amedai katika kikao hicho kwamba Iran imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayohusiana na silaha.

0 comments: