WAUGUZI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WATOA ZAWADI KWA WAGONJWA

ana
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (kushoto) akizungumza na wauguzi baada ya wauguzi hao kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo. Zawadi hizo zimepokelewa na mtoto Neema Selemani kwa niaba ya wagonjwa wengine. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Jengo la watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja na Katibu wa Tughe Tawi La Muhimbili, Bw. Faustine Fidelis.
ana-1
Baadhi ya wauguzi wakiwa katika hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wagonjwa mbalimbali.
ana-2
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Agnes Mtawa akitoa zawadi kwa mtoto Neema Selemani ambaye amepokea kwa niaba ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo, Kushoto ni Mkuu wa Jengo la watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja
ana-3
 Wauguzi wakifuatilia hafla hiyo jana.
ana-4
Mkuu wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja (katikati) akivishwa kitenge baada ya kupewa zawadi na wauguzi wenzake.
ana-5
 Meneja kutoka majengo mbalimbali katika hospitali hiyo wakiwa katika hafla hiyo jana. Kutoka Kulia ni Meneja wa Jengo la Ufuaji, Bi. Lina Kinabo, Meneja wa Jengo la Upasuaji, Bi. Jane Chuwa, Meneja wa Jengo la Huduma za Nje, Bi. Juni Samwel na Meneja wa Jengo la Sewahaji, Bi. Salome Mayenga.
ana-6
 Mkuu wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja akimkabidhi Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa zawadi maalamu.
ana-7
Bi. Anna Mponeja akimlisha keki mtoto Neema Seleman katika hafla fupi iliyofanyika  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana wametoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa amewashukuru wauguzi hao kwa kuonyesha ushirikiano katika kazi na kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa.
Mtawa aliwaasa wauguzi kuendelea na upendo huo waliouonyesha katika kipindi chote cha mwaka 2016 kwa kuwa ndio upendo ambao Mungu anataka wauonyeshe kwa wagonjwa.
Pia, aliwapongeza kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika mwaka huu na kuwataka kutumia changamoto hizo kama sehemu ya mikakati ya mwaka 2017.
Naye Meneja wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja aliwashukuru wauguzi kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa katika kipindi chote cha mwaka 2016.

0 comments: