WAISLAMU ELFU 50 WA MYANMARI WAMEKIMBILIA NCHINI BANGLADESH

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Bangladesh imetangaza kuwa, Waislamu elfu 50 wa jamii ya Rohingya huko nchini Myanmar wakimbilia katika nchi hiyo hadi sasa kujinusuru na vitendo vya ukandamizaji dhidi yao.
Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Bangladesh imeeleza kuwa, raia takribani elfu 50 wa jamii ya Waislamu wa jimbo la Rakhine kutoka katika jamii ya wachache ya Rohingya wamekimbilia nchini humo kujiokoa na vitendo vya ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi yao vinavyofanywa na mabudha wa Myanmar.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Banglaesh imemuita balozi wa Myanmar mjini Dhaka na kumuelezea wasiwasi iliyonao nchi hiyo kutokana na kuendelea vitendo vya ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa jamii ya wachache ya Rohingya nchini Mynamar.
Wakati huo huo, serikali ya Bangladesh imewataka raia laki tatu wa Myanmar wanaoishi kinyume cha sheria nchini humo kurejea makwao.
Waislamu wa Rohingya
Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa, jumuiya za misaada ya kibinadamu pia haziwasaidii Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar ambao wanazingirwa na jeshi la nchi hiyo.
Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo

0 comments: