SIMULIZI ZA KUSISIMUA : SIKU ANDY CHANDE ALIPOITWA IKULU YA JULIUS NYERERE...

Image may contain: 5 people
Ikafika siku  hiyo Andy akaitwa na rafiki yake Julius aende Ikulu. Hata alipoingia Ikulu, Andy alimwona Julius mwingine. Hakuwa mcheshi kama ilivyokuwa kawaida yake. Julius akamwambia Andy akae kitako na hapo hapo akamfahamisha maamuzi ya kutaifisha kiwanda chao na kuwa Shirika la Umma.
Na cha ajabu, Julius akamwomba rafiki yake Andy awe Mwenyekiti wa Kwanza wa Bodi ya National Milling Cooperation!
Andy akakubali! Na akaifanya kazi ile kwa nguvu zake zote.
Inasikitisha kuona leo Andy anaanikwa kwenye magazeti ya udaku na kutolewa taswira hasi. Tena ni Andy huyu huyu ambaye aliwahi kuwa mmoja wa wajumbe wa Tume iliyokuwa ikipitia filamu zote zinazoingizwa Tanzania kuziangalia kabla umma haujaonyeshwa. Lengo lilikuwa kuhakikisha kuwa filamu hizo za kigeni haziathiri maadili, mila na utamaduni wetu.
Leo Andy amekuwa mhanga wa baadhi ya vyombo vya habari vinavyokiuka maadili, mila na utamaduni wetu, kwa kumuanika hadharani, tena kwa kuweka picha zake, bila ridhaa yake, kuwa ni mwanachama wa jumuiya ya Freemasons, jumuiya ambayo, kwa kupotosha umma, media inadai wanachama wake wanaamudu mashetani!
Andy Chande hajawahi kukana kuwa mwanachama wa Freemasons. Hilo pia ameliandika kwenye kitabu chake. Ni wengi wasiojua Freemasons ni nini. Nitaliandika hili la Freemasons, na hata Andy mwenyewe anavyolielezea.
Naam, kuna waliamua kutetea uvivu wao kwa kusingizia Freemasons!

0 comments: